2 Cor 13:14

The grace of the Lord Jesus Christ, and the love of God, and the communion of the Holy Ghost, be with you all. Amen. KJV

For "Straight Talk About Being Born Again and Baptized" in Swahili click HERE!
      
 
In from Rev. Julius Ashiono:
 

“SANCTIFICATION IS IN YOU – IT IS  A PERSON HE  LIVES  IN YOU.”


Utakaso wako umeingia ndani- Yeye anaishi ndani yako !

1 Wakorintho 1:30

“Mungu ndiye chanzo cha uzima wenu katika Kristo Yesu, aliyefanyika kwetu hekima itokayo kwa Mungu na haki na utakaso na ukombozi,”

Hapa  tuna ona  ya kwamba utakaso wetu umo ndani ya  Kristo, na wakati unapo okoka basi hapa anaishi ndani  yako , kwa hivyo utakaso wako upo ndani mwako .Tena ni utakaso ni mtu , yaani Kristo anaishi ndani yetu .

 

Je umewahi kuingia kwa  nyumba ingine mara moja au zaidi maishani mwako?Je ilikupasa wewe mwenyewe  kusafisha ile nyumba kuhakikisha ya ilikuwa safi kabla ya kuingia na jamii yako kukaa ndani mle ?

Hi ni picha mzuri ya yale  Mungu alifanya kabla aingie  ndani mwako. Kuhakikisha nyumba Yake – wewe – imekuwa safi kabisa ,Alisafisha nyumba Yeye mwenyewe. Kusafisha kwake hakungekuwa mzuri sana – ila tu  ndani damu ya Yesu ingefanya hiyo kazi  kikamilifu .

Hii ni habari njema ! Wewe umesafishwa na ni takatifu – u matakatifu maana Mungu Matakatifu  ana ishi ndani yako. Waef 1:4 inasema tu  “ Kwa maana alituchagua katika Yeye kabla ya kuumbwa ulimwengu ili tuwe watakatifu na bila lawama mbele Zake.

 

Je lipi tunda la jambo hili kwamba wewe tayari umefanywa safi na Yeye, na sasa Yeye anaishi ndani yako? Hii barua ya habari njema ina mafundisho kuhusu

 utakaso,somo ambalo kwa wengine limekuwa mzigo na sababu ya kuhukumu. Walakini, Yesu alisema hakuja kuhukumu ila ni kuokoa, na  Mzigo ni mwepesi.Jinsi tumeona katika maeneo baada ya eneo , Yesu mwenyewe jawabu lake na sululisho. Je inaweza kuwa  sawa na utakaso?  Na tunaweza kumwomba Mungu kwa ya kuongezeka kwa undani na ufunuo tunavyo weza kujisomea mafundisho haya yaliyopo katika barua  hii .

 
Last message:
 
 
 ONDOKA  na USHUKE mpaka Nyumba ya Mfinyanzi

                                       Atakufinyanga Tena

                                      Yeremia  18:1-4

Maombi :

 

Yeremia 18:1-4

    Neno hili ndilo lililomjia Yeremia , kutoka kwa BWANA, kusema,

               Tambua : NENO lilimjia ( Bwana , kwa udhahiri  alimtembelea  Yeremiah)

                Tambua :  Yeremia  anatambuliwa na  Mungu… kujulikana  na Mungu

               Tambua : Hi  inadhirisha  uhusiano kati yao.

               Tambua :  Ina maanisha  Yeremia ni mtu wa kupokea. Ana weza sikia kutoka    

                                kwa sauti ya  Bwana

                Tambua : Waebrania : 13:8 Yesu Kristo ni yeye  yule, jana, leo na milele.

                               Malaki 3:6 Kwa kuwa mimi , BWANA, sina kigeugeu;

              Tambua : Alitaka  kusema na watuWake , kwa hivyo Angali ana nena leo hii

                Tambua :Yesu  anasema  habari ya Masikio yenye kusikia.

                                   Marko 4:23 Mwenye masikio na asikie!"

Alisikia nini ? Maagizo .

 Je  Mungu anaweza kuagizo  wewe na mimi? Je anaweza kutuhimiza ,Je anaweza kutia nuru  kwa  NENO Lake ?

 

Ujumbe :

2.Ondoka , ukashuke mpaka nyumba ya mfinyanzi, na huko nitakusikizisha  maneno yangu.

 

Tambua: Ondoka ! amka Yeremiah! Wewe hauko mahala sawa.Unahitaji kufanya  kitu.Unahitaji  kuenda pale ninapo weza kukutana na wewe .Enenda mahala nitakapo kufundisha.

 

Tambua : MPAKA , tuondoke  hatawezi kufika katika Nyumba ya  Mfinyanzi.Mungu  hawezi kutuleta nyumbani  Mwake , Ni sharti  tu ondoke na tuende! Lazima tumsikize Yeye  na Tuende anapo tuongoza sisi.

 

Kwa nini Anatutuma mahali Anako tutuma ?

      Kupokea toka  kwake  yale hatuwezi kupokea toka mahali pengine .

       Kuona kitu anacho taka kutuonyesha ambacho hatuwezi kuona  

        kwengineko .

      Kukutana na sisi ni   mahala  pa Upako wake maalum.

     Kufanya  kitu anacho taka kufanyia  wengine .

     Kushiriki  ujumbe wake na wengine

     Kutufanyia  matendo mema .

            Tambua: Ni sharti  tuende MWENDO HUU WOTE MPAKA  HUKO. Hatuwezi   

                            kuenda nusu tu na tuwe Nyumbani mwa Bwana !

             Tambua : Mungu  alikuwa na sababu maalum kwa nini alitaka Yeremia  aende  

                              katika Nyumba ya  Mfanyanzi . Alitaka ampe  ujumbe wa mfano., ule

                               ambao ange UONA.  Tuna hitaji  macho ya kuona pia  masikio  ya

                               kusikia .

Kumbukumbu la Torati 29 :4  lakini  BWANA hakuwapa moyo wa kujua , wala     macho ya kuona, wala masikio ya kusikia , hata leo  hivi.

 Yohana 5:19-20 :

 19.Yesu akawaambia, "Kweli nawaambieni, Mwana hawezi       kufanya kitu peke yake; anaweza tu kufanya kile anachomwona Baba akikifanya.  Maana kile anachofanya Baba, Mwana hukifanya vilevile.

 20.Baba ampenda Mwana, na humwonyesha kila kitu anachokifanya      yeye  mwenyewe, tena atamwonyesha mambo makuu kuliko haya, nanyi mtastaajabu.

 Tambua  : Yeremia  ALIPOFIKA  BILA SHAKA Mungu  akazungumza na Mtumishi  

                  akasikia

Tambua:  Kwa Yeremia alikuwa na chaguo , la kutii na   kupokea au  kutotii na  asijua

                  Mungu alikuwa  na jambo lipi  juu  yake ..Hii  ni kutosha kunifanya  mimi 

                 nitii.Ninataka kujua Mungu ana jambo lipi katika  hasina yake kwa ajili    

                 yangu!

Tambua : Kuna ahadi  hapo  Mungu anasema ata msababisha  Yeremia  kusikia !!!

               Anaweza kufanya  hivyo kwetu sisi tunapo weza  kuchagua  kumtii  Yeye.

 Tambua: Tuko karibu kuona Zawadi ya Yeremia  aliye chagua kutii maagizo ya Mungu

                 Wake .

  Tambua : Tuko karibu kuona hadithi ya  UPENDO WA  MUNGU  ukifunguliwa mbele      

                   ya  macho yetu !

 

3. Basi ni shuka  mapaka nyumbani mwa mfinyanzi na tazama, alikuwa akifanya kazi yake  kwa magurudumu.

       Tumbua : Mfinyanzi katika  hadithi  hii ni  Baba Mungu . Yeye  anafinyanga

                       chombo,   Yeremia aliweza  kuona  hali ya upitilzo wa Mwanadamu, aliye   

                      chombo .

      Tambua : sisini kazi ya  Mikono  ya  Mungu. Waef 2:10 Sisi ni viumbe vyake 

                       Mungu, na kwa kuungana na Kristo Yesu, alituumba kwa ajili ya

                        kuishi maisha ya matendo mema aliyotutayarishia tuyatende.

      Tambua: Yeye ni Mwanzo tena  mwisho . Ufunuo 21:6

                        Kisha akaniambia, "Yametimia! Mimi ni Alfa na Omega, Mwanzo na Mwisho. Aliye na kiu nitampa kinywaji cha bure kutoka katika chemchemi ya maji ya uzima.

 Tumbua : Tunayo ahadi yake ya kwamba alicho anza ata  kamilisha

 Wafilipi 1:6 Nami niliaminilo ndilo  hili, ya kwanba yeye  aliyo anza kazi moyoni mwenye  ataimaliza hata siku ya  Kristo Yesu .

 

 

 

 

 

 

4. Na chombo kile alikuwa akifinyanga, kilipoharibika mkononi mwake yule mafinyanzi,alikifanyiza tena kuwa chombo kingine, kama alivyoona vema yule mafinyanzi kukifanya.

     Tambua :  Chombo alichokifanya …. Mkristo .alitengenezwa na Mungu . Sura ya 

                       mfano wake .

 Tambua:Tuliumbwa kwa udongo. Ingekuwaje kwamba hili  umbo lingekuwa  udongo.Udongo unafinyangwa, unayo rangi, kitu kinacho weza kufanyazwa .Udongo hauwezi kujiumba . Ila sharti  upokee  mshurutisho  kutokana na vitu  vilivyo karibu nao .Mungu alimwumba mwanadamu toka  kwa mavumbi  ya nchi kwa mikono Yake .Yeye  ndiye aliweza kuwa  bayana   ya kufanya umbo la mwanzo la chombo hiki . Yeye  ndiye atakaye kuwa  bayana ya  kufanya  uamuzi wa  mwisho juu  ya chombo  hiki .

  Tambua : Mavunbi HAYAWI  KITU ila  mavumbi  MPAKA YEYE( mfinyanzi 

                    anapo ushika na kuufanyiza. Shukuru Mungu kwa mguso wake.

   Tambua : Mungu anataka KUGUSA watu Wake

    Tambua : Mungu ALITUUMBA SISI KWANZA , alafu Akapuliza UHAI ndani yetu,

                     na ROHO  WAKE akatufanya kuwa  haya hai. Huo  uhai sharti ulitakikana

                     uwe wa milele, lakini  dhambi  iliweza kuharibu na kulete mauti .

 

      Tambua : Tangu dhambi  na mauti  zimeingia katika dunia lazima tukabiliane na mvuto mwingine juu ya  maisha yetu, mzongo kuliko  Mungu . Licha  ya kuwa mikononi Mwake tukiwa Wake, tungali twaishi katika mwili ,duniani hapa .Tuna kumbwa na mzongo katika pande  zote .Misiba hutukia.Vipande na sehemu ya  yaliyopita  wakati mwingine  yamesababisha sisi kuvunjika  moyo na kukosa kufanya kazi vizuri na tuna patwa na dhambi .Ni wakati  tunapo umika KIKAMILIFU mikononi  Mwake ndipo tunakuwa salama 

 

Tambua   :  Kila chombo ni cha  kipekee . HUKUNA vyombo viwili wanavyo fanana . Kila chombo kina thamana yake . Kina  mwenyewe , mfinyanzi . Sisi ni Vyombo vya Mungu Maalum .Anataka kutotoa  kutoka utukufu hadi  utukufu ,  Akivirembeshe vyombo vyetu hadi milele.

2 Wakorintho 3:18

Basi, sisi sote ambao nyuso zetu hazikufunikwa, twaonyesha kama katika kioo, utukufu wa Bwana; tunabadilishwa tufanane zaidi na huo mfano wake kwa utukufu mwingi zaidi. Hiyo ni kazi yake Roho wa Bwana.

 

Tambua  : Udongo uliwaza kuharibiwa , Kuna uzito fulani  ulioweza kuufinya

                   ULIPO KUWA MKONONI MWAKE .

Tambua : Wakati mwingine  tunaumizwa licha  ya kuwa  mikononi Mwake .Tambua  ahadi iliyopo hapa  Ali UFANYA  TENA  UDONGO HUO. Hakuwacha udongo  huo  chombo kilicho vunjika au  kilicho  haribiwa . Hakuwacha kuwa bure . Hakuwacha kuwa sura mbaya  na kuwa bure.

 

Kwa kila  kuanguka,kwa kila masaibu katika  maishani  mwetu , kwa kila dhambi iliyo njiani mwetu , kwa kila wakati tunopo danganyika , Yeye  anataka kutuumba  tena , mara ingine .  Sisi  ni udongo ule ule , chombo kile , Lakini Atatufinyanga  tena kuwa, chengine , chombo  bila  hitalafu , ule uhuribifu .Kila wakati kwa subira hutufinyanga sisi, na tuta remebeka  zaidi katika Yeye , na uhakika zaidi, uaminifu  zaidi , zaidi tukiwa na hasina , zaidi tunao stahili  kuaminika kumfuata Yeye.

                         Ni jinsi  gani Anatenda kazi  kwa mapito ya njia  ya  maisha yetu .

 

 Muhtasari :

 Tuna hitaji KUONDOKA

 Tuna hitaji KUENDA kwa Nyumba ya  Mungu

 Yeye ata Tunenea na Kusababisha Kusikia

 Yeye  ndiye Mwanzo wetu  na Yeye ata enda nasi mpaka  Mwisho .

  Yeye  hatatuwacha sisi  wala kututupu .

 

Waeb  13:5-6

 5.Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: "Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa."

6 Ndiyo maana tunathubutu kusema: "Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?"

 

Kwa  kila uharibisfu maishani mwetu , Yeye  ata tufinyanga  upya , IWAPO TUPO

MIKONONI MWAKE.

Tuna hitaji  kuchagua KUDUMU KATIKA USALAMA WA MIKONO  ZAKE.

Wakati wa maombi .

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 
In from Rev. Julius Ashiono:
 
 
Website Powered by Community Spice